Vijana wawili raia wa Philippines wamejikuta katika hati hati ya kuokoa maisha yao baada ya kukimbizwa na mtoto wa tembo walipokuwa wanakatiza katika hifadhi ya wanyama pori na pikipiki.
Katika pilika pilika za kuokoa maisha yao walijikuta wakiicha pikipiki waliokuwa wamepanda na kuanza kukimbia mbali na mtoto wa tembo huyo aliekuwa anawakimbiza.
Ambapo hata hivyo tembo huyo hakuwakimbiza sana hivyo hawakudhurika pia pikipiki yao ilikuwa salama na baadae baada ya tembo huyo kukimbilia msituni waliifuta pikipiki yao na kuendelea na safari.
Eneo hili la hifadhi ya wanyama limekuwa si salama sana kwa watu wanaokatiza kwani wanyama pori hasa tembo wamekuwa wanatishia amani watu mbali mbali hata kudiriki kuwajeruhi watu na mali zao zikiwemo vyombo vyao vyamoto gari na pikipiki.
Post a Comment