Wanawake wawili mtu na rafiki yake wamejikuta wanaingia kwenye aibu kubwa ya kuvuliwa nguo zao zote kwa kuchaniwa na watu na wakitembea wakiwa uchi wa mnyama kwa kile kilichodaiwa kuvaa nguo fupi ambazo zinawaonesha miili yao.
Tukio hilo lilitokea nchini Uganda hivi karibuni ambapo inadaiwa wanawake hao walionekana wakitembea mtaani mchana kweupe huku wakiwa wamevalia nguo fupi ndipo walipojikuta wanashushiwa ghalika na wanaume ambao hawakupendezwa na uvaaji wa nguo zao na kudai kuwa si za heshima na hazina maadili kwa jamii ya kiafrika.
Kampeni kabambe sasa imeenea nchini uganda kwa kuwavua wanawake nguo kwa kuwachania kwa ambaye ataonekana amevaa nguo ambayo si ya heshima kwa jamii.
Post a Comment