Kila kukicha kumekuwa na mambo ya kukemewa kuhusiana na suala zima kujichukulia sheria mkononi, lakini bado kuna matukio mengi ya kujichukulia sheria mkononi ambayo yanazidi kutokea.
Hivi karibuni nchini Congo wanajeshi wa nchi hiyo walijumuika na raia wa kawaida kujichukulia sheria mkononi kwa kumpiga mtu mmoja alietuhumiwa kuwa ni kibaka aliemkwapulia mama mmoja simu yake ya mkononi.
Suala la kustaajabisha katika tukio hili ni pale kibaka huyo alipokuwa akipigwa huku anakimbia na alipowaona wanajeshi hao aliwakimbilia kwa kudhani ingekuwa ni msaada wa kisheria kwao lakini na wao walikutwa wakishirikiana na raia wa kawaida kumpika kibaka huyo kwa mawe pia kumchoma na vitu vyenye ncha kali hadi kumsababishia kupelekea kifo.
Tukio hili limestaajabisha wengi na hadi kufikia hatua kupoteza matumaini na jeshi la nchi hiyo kwa kitendo chao kibaya walichomfanyia raia huyo ambaye alikuwa akisemekana alikuwa ni mwizi.
Post a Comment