Takwimu zilizotolewa na TACAIDS Mwaka jana
Tarehe 1 Disemba, siku ya UKIMWI duniani.Ilikuwa ikionesha kasi ya
maambuziki ya ugonjwa hatari wa ukimwi katika nchi yetu ya Tanzania na Mkoa wa
Dar es salaam ukiwa unashikilia nafasi ya sita(6) kwa maambuzi ya ugonjwa huo, huku wakitoa rai
mbalimbali kwa jamii kupunguza kuwa waaminifu kwenye mahusiano, matumizi ya kondomu na njia nyingine mbalimbali.
Licha ya Rai mbalimbali kutolewa na
TACAIDS mwaka jana lakini jamii zetu bado zinaonekana kutojali hayo yote na kasi ya
maambukizi ya ugonjwa huo ikionekana kuendelea siku hadi siku.
Kasi hiyo ya maambukizi ya ugonjwa huo
hatari imejitokeza pale mama mmoja mkazi wa mikocheni B jijini Dar es salaam
aliebainika kuna na ugonjwa huo na kuusambaza kwa makusudi kwa mtu yeyote
anaemlaghai kimapenzi hasa vijana. Ilibainika kuwa mama huyo ni mjane anaeishi
na watoto wake wawili maeneo ya mikocheni alisikika sehemu mbalimbali kuwa
ataendelea na kuwaambukiza kwa makusudi hasa vijana na watu wengine wote
watakao kuwa wanamtaka kimapenzi wala hato wakatalia.
Hali hii inasikitisha sana, watu wote mpatapo
taarifa hii hasa vijana muwe macho na kuamini ugonjwa huu hatari upo na kuna
watu wengi tunaoishi nao kwenye jamii zetu wanafanya ufedhuli kama huu wa kuwaambukiza
watu magojwa kwa makusudi.
Tuweni makini
UKIMWI UPO NA UNAUA!!
Post a Comment