Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Diamond Platinum amekutwa hivi karibuni mitaa ya tandale akila mishikaki ya kuchoma kwa vijiti akiwa yeye na Babu Tale.
Tukio hili lilijitokeza baada ya Diamond kutembelea maeneo ya huko kwao alikokuwa anaishi zamani akiwa ameambatana na babu tale ndipo alipoona mishikaki kwa kijana mmoja ambaye alidai kabla hajatoka kimuziki ni sehemu ambayo alikuwa anapenda kwenda kula mishikaki hiyo "Kabla sijatoka kimuziki hii sehemu nilikuwa na husika sana kula hii mishikaki kwa dogo saidi ni mitamu sana, naona ladha yake bado ni ile ile bado inabamba" alisema Diamond.
Mwenye asili haachi asili akiacha asili hana akili, Diamond mbali na ustaa wake hakusita kufanya kile kilichokuwa asili kwake alipokuwa anafanya hapo awali.
Post a Comment