Mashabiki wamejitokeza kwa wingi kushuhudia pambano la ngumi za kulipwa kati ya Floyd Mayweather na Mfilipino, Manny Pacquiao.
Mashabiki kutoka sehemu mbalimbali nchini Ufilipino waliacha kazi zao kwa ajili ya kushuhudia pambano hilo lililokuwa likipigwa Las Vegas nchini Marekani.
Kutokana na tofauti ya muda, wakati Las Vegas ilikuwa usiku, Ufilipino ilikuwa ni mchana jua kali na mashabiki waliacha kazi zao ili washuhudie pambano hilo katika sehemu mbalimbali za wazi.
Wengi walikuwa wakishangilia kwa nguvu, lengo likiwa ni kuona Pacquiao anashinda.
Hata hivyo, mwisho shujaa wao ambaye ni mmoja wa wanasiasa wanaopendwa nchini humo, alipoteza kwa pointi.
Post a Comment