Msanii wa nyimbo za Bongo Fleva Abdul Nasib maarufu kwa jina la Diamond Platnum anataraji kutoa wimbo wake mwingine mpya aliowashirikisha wanamuziki wa kinigeria Paul na Peter P-square wanaofanya kazi zao za muziki nchini marekani.
Muziki huo mpya wa diamond platnum kwasasa uko tayari na yeye mwenyewe amesema hivyo na kusema kuwa siku ya kuziki huo kutoka anawaachia mashabiki wake waseme wangependa utoke lini.
Hii ni kwa mara ya pili sasa Msanii Diamond Platnum kufanya kazi ya muziki na wanamuzi hao raia wa Nigeria P-square ambapo muziki wa kwanza ambao Diamond alifanya na P-square ulikuwa unaitwa NAKUPENDA ambao ulitoka mwaka jana 2014.
Post a Comment