Mke akiwa na kipaza sauti akimtangaza mumewe kumfumania na mchepuko
Kuwa uyaone ndio msemo wa wawatu wazima, tembea uone mengi ni msemo wa wawale wanao kaa tu pahala pamoja na kutotembea kujionea mambo kwani mkaa bure si sawa na yule mtembea bure.
Katika zile harakati za mwanahabari wetu wa mtembea bure na kuzunguka huku na kule kung'aza ya dunia amejikuta anakutana na sauti iliyosikika kusikika kwenye vyombo vya redio na televisheni kwa njia ya matangazo lakini hili halikuwa tangazo kutokana na kulindima idadi kubwa ya watu na wengine wakiwa na simu zao za kisasa(smartphone) wakionekana kuchukua tukio hilo kwa umakini kwa picha za sili na mnato kuhakikisha tukio hili haliwapiti hata.
Ule msemo wa michepuko sio dili baki njia kuu ulisikika ukipaza kwa sauti kubwa hivi karibu kuko maeneo ya keko magorofani ni baada ya mama mmoja kumfumania mumewe na mchepuko na kujikuta akichezea kipigo huku aliishia kutembezwa mtaa mzima kwa kipaza sauti na maneno hayo ya "mchepuko sio dili baki njia kuu" ulitawala mdomoni mwa mama huyo.
Mama huyu aliamua kumfanyia haya mumewe kwa kusema kuwa liwe fundisho kwa wanaume wengine wenye tabia kama alizokuwa nazo mumewe, kwani awali alipodokezwa na watu kuwa mumewe anachepuka hakuamini alijua tu ni maneno ya watu ya kutaka kuchafua ndoa yao lakini hakusita kulifatilia jambo hilo na ndipo alipokuja kujua ukweli na kuamua kufanya hv ili iwe fundisho kwa wengine.