![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj5-BW8rxPdZBMGg1iqiTFDTNghgVGLOndUBn0EDVSGISdtaxrPjVa7ZJ3mJO_4L7pNM0z_teyXjCxnYDwYhiq8NFD8TzB_ZnzWs1V7TdMYh6W1K6t7XFs_z1ZuYJykNEnSMaqI7McAv94/s640/tcra1+-+Copy.jpg)
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA ambayo iko chini ya Wizara ya Mawasilino, Sayansi na Teknolojia imeanza kufatilia watu wanatumia mtandao vibaya kwa kuweka vichochezi mbalimbali, matusi na picha chafu ambazo si nzuri kwa jamii.
Sheria hiyo ambayo ilisainiwa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia tarehe 14 mwezi Agosti mwaka huu na kuruhusiwa kuanza kutumika Tarehe 1 Septemba mwaka huu ambayo ni leo. Sheria hii ya matusi ya mtandaoni imezingatia zaidi matumizi mabaya ya kimtandao ikiwemo kutuma picha za kizushi, maneno ya kizushi, matusi na video chafu mtandaoni.
Sheria itamgusa yeyote atakaekiuka hayo na kutoza faini ya kuanzia Tsh 3,000/= na kuendelea kulingana na ukubwa wa kosa lenyewe.
Get Free Email Updates to your Inbox!
on Tuesday, September 1, 2015
Post a Comment