Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Huu ndio ushauri ulotolewa na TCRA juu ya sheria ya Matusi ya Kimtandao ilioanza kutumika rasmi jana.

Mamlaka ya mawasiliano nchini Tanzania TCRA imetoa ushauri kwa watanzania wote juu ya sheria ya matusi ya mtandaoni ambayo imeanza rasmi septemba 1.
Ushauri wa TCRA ulotolewa kwa wananchi juu ya sheria ya matusi ya mtandaoni ni kuwa undapo utatumiwa video, sauti au hata picha ambayo si nzuri kwa jamii na inayoleta vichochezi kwa jamii ni vyema uifute na sio kuisambaza kwa watu wengine.

Hivi ndio vipengele vya sheria ya matusi mtandaoni ambavyo usipokuwa makini vinaweza kukufunga, vijue hapa.

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA ambayo iko chini ya Wizara ya Mawasilino, Sayansi na Teknolojia imeanza kufatilia watu wanatumia mtandao vibaya kwa kuweka vichochezi mbalimbali, matusi na picha chafu ambazo si nzuri kwa jamii.

Sheria hiyo ambayo ilisainiwa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia tarehe 14 mwezi Agosti mwaka huu na kuruhusiwa kuanza kutumika Tarehe 1 Septemba mwaka huu ambayo ni leo. Sheria hii ya matusi ya mtandaoni imezingatia zaidi matumizi mabaya ya kimtandao ikiwemo kutuma picha za kizushi, maneno ya kizushi, matusi na video chafu mtandaoni.

Sheria itamgusa yeyote atakaekiuka hayo na kutoza faini ya kuanzia Tsh 3,000/= na kuendelea kulingana na ukubwa wa kosa lenyewe.
Powered by Blogger.

www.CodeNirvana.in

float ads


© Copyright UHAKIKA WA HABARI
Back To Top